SNOOP DOGG ni kama amechoka Hip-Hop hivi, Rapper huyu mwenye umri wa miaka 40 sasa, mwenye jina halisi laCalvin Broadus Jr., anaamini ni kama amezaliwa upya baada ya kutembelea JAMAICA mwezi Januari/Februari na kusema kuwa, kwa sasa yupo tayari kutengeneza muziki ambao watoto na wazee wanaweza kuusikiliza. Msanii huyu anaefahamika vizuri kwa kufanya muziki wa kufoka foka yaani 'Rap' na unaotafsiriwa kuwa ni wa kihuni, anaamini kuwa kama Bob Marley mpya na yuko tayari kuimba na kuushika muziki wa Reggae badala ya Tamaduni za Bunduki alizokuwa anaimba kabla. Katika kufanya vyote hivi, SNOOP DOGG amebadili jina na sasa anajiita SNOOP LION na pia alipewa jina la "Berhane" lenye asili ya Ethiopia likimaanisha "Mwanga wa Dunia". Baadae mwaka huu, SNOOP LIONataachia album yake "Reicarnated" yenye mahadhi ya Reggae. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumatatu hii, jiji New York, Snoop Lion aliyasema hayo ikiwa ni pamoja na kucheza ngoma zake tano, moja ikimshirikisha manae wa k*** inayojulikana kama "NO GUNS ALLOWED".
Album hiyo itayofuatiwa na documentary itakayofahamika kwa jina hilo hilo hilo, ikimuonesha yeye akitengeneza muziki ikiwemo mambo mengine ya karibu yanayohusisha maisha yake. Album itazinduliwa katika Tamasha la "Toronto International Film Festival" mwezi Septemba.
©Mkimya Ent.